MANGE KIMAMBI NI KAMA MBWA KOKO, MUOGA KULIKO WATANZANIA WOTE. KINACHOMPA JEURI NI SABABU YUPO NJE YA TANZANIA
Kutoka kwa mdau wa siasa;
Nimefuatilia kwa makini sana na pia mimi ni mfuasi mkubwa wa mange.
Maneno yake ni uhamasishaji wake katika kuikomboa siasa au demokrasia ya Tanzania hakuna mtu aliyefanikiwa kuwashawishi watanzania wengi kama mange. Nampongeza sana anavyowafumbua macho na kuwapa ujasiri mpaka watu wanapata confidence kwamba wanaweza kumuondoa raisi madarakani.
Kinachonifanya nimuone mange ni kama mbwa koko ambaye jeuri yake ni akiwa kwao tu ni kwamba vyote anavyofanya anavifanya akiwa marekani.
Anaikosoa serikali akiwa marekani.
Anatukana wanasiasa akiwa marekani
Anawahamasisha watu wajitokeze barabarani waandamane wakati yeye ana uhakika wa asilimia 100 kwamba yeye na familia yake wapo salama huku nyinyi mnapigwa virungu na mabomu ya machozi.
Watanzania lazima mjiulize maswali marahisi sana.
Hivi huyu mange kama ana ujasiri wa kuipigania Tanzania kwanini asije kuungana nanyi katika maandamano, migomo na harakati zote badala ya kuandika tu instagram?
Jibu ni rahisi
Anajua akija watakachomfanya na hayupo tayari kujitoa kupigwa, kuumizwa au kupata lolote baya kisa kuikomboa demokrasia.
Kwa kifupi ni muoga
Anaogopa kuumia maana anajua gharama halisi ya kufanya anayowahamasisha muyafanye.
Sasa wewe ingia kichwakichwa kwa kufuata maneno ya mtu ambaye hata yeye mwenyewe hawezi kufanya mambo anayowahamasisha nyinyi mfanye akiwa Tanzania.
Anaishia kuandika tu insta kitu ambacho kila mtu angekiweza angekuwa nje.
Amini nawaambia mange angekuwa Tanzania hata hizo post zake asingeandika yani angekuwa mpole na angeisupport serikali ili alinde tumbo lake.
Mkitaka mumpatie mange mwambieni siku ya maandamano tunakutaka nawewe muhamasishaji wetu uwepo na uongoze msafara.
Uone kama hajakublock.
bongolifestyle.blogspot.com

No comments: